Home KIMATAIFA TANZANIA YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

TANZANIA YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

0

IKIWA ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuingia kwenye Kombe la Dunia kupitia timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17, Serengeti wamefanikiwa kutnga hatua ya robo fainali.

Mchezo wa leo Oktoba 18 ambao ulikuwa ni watatu kwa Tanzania imeambulia sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Canada.

Kwenye mchezo wa leo ni Canada walianza kupata bao la kuongoza ilikuwa dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Allen na liliwekwa usawa na Veronica Mapunda dakika ya 35.

Inatinga hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 4 kwa kuwa ilipata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Ufaransa na ilipoteza mchezo mbele Japan kwa kufungwa mabao 4-0.

Pongezi kwa vijana kwa kazi nzuri iliyofanyika Uwanja wa Patil Navi Mumbai.

Mikono ya kipa namba moja wa Tanzania inayonolewa na Bakari Shime Zulfa Makau ilikuwa imara kwenye kuokoa michomo ya Canada.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here