Mkurugenzi wa michezo wa Shakhtar Donetsk Carlo Nicolini anasema Arsenal na Manchester City ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyotaka kumnunua mshambuliaji wa Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21, ambaye anaweza kugharimu zaidi ya euro 100m ambayo Manchester United ililipa Ajax kumnasa mshambuliaji wa Brazil Antony. (Calciomercato.it, via Mirror)
Newcastle United wanatarajiwa kumpa mchezaji wa kimataifa wa Paraguay Miguel Almiron, 28, mkataba mpya kufuatia kuimarika kwake chini ya meneja Eddie Howe. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg pia yuko mbioni kuongezewa mkataba mpya, huku Tottenham ikionyesha kuwa wanataka kuanza mazungumzo juu ya masharti mapya ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Times)
Kiungo mshambuliaji wa Sporting Lisbon Marcus Edwards, 23, anasema uhamisho wa kwenda Ureno umekuwa mzuri kwake lakini angependa kurejea kucheza katika nchi yake ya England. (Evening Standard)
Fulham wamewasilisha ombi la pili kwa kiungo wa kati wa Brazil Pablo Maia, 20, na pia wanawafuatilia viungo wa Sao Paulo Rodrigo Nestor, 22, na Igor Gomes, 23, pamoja na beki wa kati Luizao, 20. (HITC).
Nottingham Forest pia wanavutiwa na Maia na wako tayari kulipa bei ya pauni milioni 9 kwa kinda huyo wa Brazil. (Nottinghamshire Live)
Manchester United inamfuatilia mlinda mlango wa Porto wa Ureno Diogo Costa, 23, na mlinda mlango wa Athletic Bilbao na Hispania Unai Simon, 25, wakati ikisubiri kuamua iwapo wataongeza mkataba wa mchezaji wa kimataifa wa Hispania David de Gea, 31. (Athletic)
Southampton na Leicester City zinamfuatilia kwa karibu nyota wa Toulouse na mchezaji wa kimataifa wa Morocco Zakaria Aboukhlal, 22. Winga huyo anatarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar. (Echo)
Meneja mpya wa Aston Villa Unai Emery atapewa fedha nyingi kuimarisha kikosi chake wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)
Mshambulizi wa Liverpool Darwin Nunez, 23, anasema mchezaji mwenzake wa Uruguay Luis Suarez, 35, ambaye pia alichezea Reds, aliwasiliana naye ili kumpa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na presha ya kucheza Ligi kuu England. (ESPN)
Rais wa Lazio Claudio Lotito anasema kiungo wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic hatauzwa na atapewa ofa ya kuongezewa kandarasi, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika timu hiyo ya Serie A unamalizika mwaka 2024. (Il Messaggero).
Meneja wa QPR, Michael Beale alikataa nafasi ya kuwa mkufunzi wa Wolverhampton Wanderers kwa sababu ya “mzozo” ambao yangehusishwa na kuhama kwake. (Telegraph)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE