Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS (13.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS (13.10.2022)

0

Manchester City wameziambia klabu kadhaa – ikiwa ni pamoja na Bayern Munich na Inter Milan – ambazo zimeulizia kuhusu upatikanaji wa mlinzi wa Uholanzi Nathan Ake kwamba haitamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mwezi Januari. (90Min)

AC Milan wanajiandaa kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao na wangependa kufikia muafaka kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia.

Chelsea wamekuwa wakihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na wanafuatilia mazungumzo hayo kwa karibu. (La Gazzetta dello Sport)

AC Milan wanavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 26, ambaye mkataba wake na The Blues unafikia kikomo mwaka 2024. (Calciomercato).

Chelsea wanakaribia kufikia makubaliano ya kumteua mkuu wa usajili wa Southampton Joe Shields kama mkurugenzi wao wa masuala ya usajili. (Guardian) 

Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Guido Rodriguez, 24, kabla ya dirisha la uhamisho la Januari. (Estadio Deportivo)

Manchester United wameripotiwa “kuongeza nguvu za kumsaka mlinda mlango wa Benfica Odysseas Vlachodimos na wanataka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki, 28, ambaye pia anasakwa na Leicester City. (Sportime )

Brentford wameanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa England Ivan Toney, 26, ambaye anahusishwa na Tottenham. (Football Insider)

Leeds United iko tayari kumpa mkataba mpya ulioboreshwa kiungo wa kati wa Uingereza Jack Harrison, 25, ambaye alikuwa anasakwa na Newcastle United katika dirisha la msimu wa joto. (Football Insider)

Wolverhampton Wanderers wapo kwenye mazungumzo ya kina na kocha wa zamani wa Olympiakos, Pedro Martins, ambaye hivi majuzi alishindwa kuafikiana kuhusu kuwa kocha wa Hull City, huku klabu hiyo ya Molineux ikitafuta mrithi wa Bruno Lage aliyetimuliwa. (Maisfutebol)

Wolves pia wamemfanyia usaili mchezaji wa zamani na bosi wa zamani wa Watford Rob Edwards kushika nafasi hiyo. (Telegraph)

Beki wa kulia wa Chelsea na England Reece James, 22, ana matumaini kwamba jeraha la goti alilopata si baya sana kufuatia tathmini ya awali. (Telegraph)

Meneja wa Lazio Maurizio Sarri hajafurahishwa na ripoti zinazomhusisha kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kuhamia Juventus. (Football Italia)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here