Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS (6.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS (6.10.2022)

0

Arsenal wanafuatilia hali ya Marcus Rashford katika klabu ya Manchester United kabla ya kutoa ofa ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)

Klabu ya Southampton iko tayari kumfuta kazi meneja Ralph Hasenhuttl baada ya klabu hiyo kuanza vibaya msimu huu. (Telegraph – subscription required)

Bosi wa Nottingham Forest Steve Cooper ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Hasenhuttl huko St Mary’s. (Mail)

Forest wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Leicester City kumpata Rafael Benitez kama meneja wao mpya, ikiwa wataamua kumtimua Cooper. (Football Insider)

Kocha mkuu wa New York Red Bulls Gerhard Struber pia anaangaziwa na Forest. (Sun)

Liverpool watafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Bayern Munich Jamal Musiala mwenye umri wa miaka 19 wa Ujerumani iwapo watashindwa kumpata kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Guinea Naby Keita, 27, hatajadili mkataba mpya na Reds hadi Januari. Mkataba wake wa sasa unaisha msimu ujao wa joto. (Bild)

Barcelona wamekubali kumuuza kabisa Antoine Griezmann, 31, kwa Atletico Madrid kwa nusu ya bei yake ya euro 40m. Fowadi huyo wa Ufaransa kwa sasa yuko kwa mkopo Atletico. (Marca – in Spanish)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 23, atakuwa analengwa zaidi na Chelsea katika dirisha la uhamisho wa 2023. (90min)

Everton watalipa pauni milioni 4.5 pekee kubadilisha mkopo wa beki wa Uingereza Conor Coady, 29 kutoka Wolves kuwa mkataba wa kudumu kabla ya mwisho wa msimu. (Telegraph – subscription required)

Lionel Messi bado hajapokea ofa zozote za kandarasi na mkataba wake wa Paris St-Germain unamalizika mwishoni mwa msimu huu, ingawa klabu ya zamani ya Barcelona ina nia ya kutaka kumsajili tena mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33. (Fabrizio Romano)

Meneja wa zamani wa Olympiakos Pedro Martins, ambaye alihusishwa na kazi ya kuifunza Wolves, anakaribia kuteuliwa kuwa meneja wa Hull.. (Talksport)

Kundi la Marekani LAMF Global Ventures Corp limeonyesha nia ya kutaka kuichukua mikoba ya Everton lakini mpango huo haufikiriwi kutimia hivi karibuni. (Liverpool Echo)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here