Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA (7.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA (7.10.2022)

0

Mshambulizi wa Norway Erling Haaland, 22, anapokea pauni 865,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester City. (Mail)

 Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekanusha uvumi kwamba Haaland ana kipengele cha kutoka ambacho kitamruhusu kujiunga na Real Madrid. (Mirror)

Galatasaray inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo ,37 mwezi Januari (Fotomac – in Turkish)

Kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante, 31, anaamini kuwa Chelsea hawataki kumuongezea mkataba, huku mkataba wake wa sasa ukikamilika msimu ujao wa joto. (Footmercato – in French)

Arsenal wanavutiwa na Porto na mshambuliaji wa Iran mwenye umri wa miaka 30 Mehdi Taremi. (A Bola, via TEAMtalk)

Real Madrid wanamfuatilia beki wa Benfica Mreno Antonio Silva, 18. (Calciomercato – in Italian)

Nyota wa Argentina Lionel Messi anasema Qatar 2022 ‘hakika’ itakuwa Kombe lake la mwisho la Dunia

Inter Milan wanatumai kupata mustakabali wa muda mrefu wa Hakan Calhanoglu katika klabu hiyo baada ya kukataa kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uturuki mwenye umri wa miaka 28 kutoka vilabu vikiwemo Everton. (TEAMtalk)

Bilionea wa Marekani Bill Foley, mmiliki wa kampuni ya NHL ya Vegas Golden Knights, ana makubaliano ya mdomo ya kuinunua Bournemouth. (Athletic – subscription required)


Mtendaji mkuu wa Bayern Munich Oliver Kahn anasema miamba hao wa Bundesliga walifikiria kumnunua Ronaldo katika majira ya joto (Bild, via Mail)

 Wolves wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Julen Lopetegui wikendi hii, kufuatia meneja huyo wa zamani wa Uhispania kutimuliwa kama kocha mkuu wa Sevilla. (Sky Sports)

 Makamu wa rais wa Barcelona ameonya kuwa bili ya mishahara ya klabu hiyo haitafikia viwango vinavyoweza kusimamiwa hadi kandarasi za majina ya nyota wakiwemo mabeki wa Uhispania Gerard Pique, 35, na Jordi Alba, 33, na kiungo Sergio Busquets, 34, kukamilika. (Mail)

Mchezaji wa zamani wa mchester United Rio Ferdinand ameitaka klabu yake ya zamani Manchester United kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, 19, ambaye pia analengwa na Real Madrid na Liverpool. (Mirror)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here