Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE (18.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE (18.10.2022)

0

Mchezaji anayelengwa na Manchester United Joao Felix, 22, azua hali ya wasiwasi katika klabu ya Atletico Madrid na mkufunzi wake Diego Simeone, na huku klabu hiyo ya Uhispania ikisisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa Ureno hauzwi, wakala wake Jorge Mendes anamtafutia klabu nyengine atakayojiunga nayo 2023. (Here We Go podcast)

Aston Villa wanavutiwa na meneja wa zamani wa Tottenham na Paris St-Germain Mauricio Pochettino kama mbadala wa Steven Gerrard. (Telegraph – subscription required)

Meneja wa Chelsea Graham Potter anatamani kuungana tena na fowadi wa Brighton Leandro Trossard, 27, huko Stamford Bridge, huku mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Seagulls Dan Ashworth pia anataka kumleta mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji Newcastle. (90 min)

Simeone pia anasema Atletico haipaswi kufikiria kumsajili fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United mwezi Januari kwa sababu ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 37 na klabu yake ya zamani ya Real Madrid. (Tigo Sports, via Metro)

Kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante bado hajafikia makubaliano na Chelsea kusaini mkataba mpya na kuna hisia kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anaweza kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao. (Fabrizio Romano)

Wakala wa mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United na Arsenal, anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 23 hana nia ya kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A. (Goal)

Wolves wamemhoji aliyekuwa Lyon, Bayer Leverkusen na bosi wa Borussia Dortmund Peter Bosz kama mgombeaji wa nafasi yao ya umeneja. (Telegraph – subscription required)

Hatua ya Chelsea ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao imepata pigo baada ya mkurugenzi wa AC Milan Daniele Massaro kusema kwamba watakutana na babake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 katika sherehe za Ballon d’Or Jumatatu ili kujadili mkataba mpya. (Express)

Fowadi wa Brazil Neymar, 30, huenda akakosa mchezo wa Paris St-Germain wa Ligue 1 dhidi ya Ajaccio Ijumaa kwa sababu ameratibiwa kutoa ushahidi mahakamani kutetea kesi yake kuhusu uhamisho wake wa 2013 kutoka Santos kwenda Barcelona (Football Transfers)

Brentford wameanza mazungumzo na meneja Thomas Frank kuhusu mkataba mpya, miezi tisa tu baada ya kusaini mkataba wake wa sasa. (Telegraph – subscription required)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United na Uingereza Michael Carrick, 41, amefanya mazungumzo zaidi na Middlesbrough na anatazamiwa kuteuliwa kuchukua nafasi ya Chris Wilder, ikiwa ni hatua yake ya kwanza ya muda wote katika uongozi. (Mail)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here