Rais wa Barcelona Joan Laporta anataka kumrejesha mshambuliaji wa Paris St-Germain Lionel Messi katika klabu hiyo ya Uhispania mwezi Januari lakini uhamisho wowote wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 utakabiliwa na vikwazo kadhaa mbeleni. (Sport)
Messi ataamua kuhusu mustakabali wake baada ya Kombe la Dunia na hataondoka PSG Januari hata kama ataamua kutosaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Ligue 1. (Ben Jacobs)
Mkataba wa kiungo wa kati wa Chelsea N’Golo Kante katika klabu ya Chelsea unakamilika msimu ujao wa joto na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 analengwa na Barcelona huku klabu hiyo ya Nou Camp ikitafuta atakayejaza pengo lililoachwa na Mhispania Sergio Busquets, 34. (Relevo – kwa Kihispania).
Sporting Lisbon wako tayari kuwasilisha ombi kwa Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, kwa mara ya pili. (Sunday Mirror)
Kiungo wa kati wa Ajax na Mexico Edson Alvarez, 25, anasema “alisikitishwa” na uhamisho wa kwenda Chelsea msimu wa joto haukutimia baada ya The Blues kuwasilisha ombi la kuchelewa kumnunua. (ESPN, via 90 Min)
Barcelona wanatarajia kumuuza mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay mwezi Januari, huku klabu Juventus ya Italia ikinyesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sport)
Kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 25, hajafurahishwa kutoshirikishwa katika kikosi cha kwanza akiwa Barcelona na anataka kurejea Serie A nchini Italia, ambako alichezea AC Milan. (Fichajes – kwa Kihispania)
Manchester City wanajiandaa kumpa kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 28, mkataba mpya wa miaka mitano kwa masharti yaliyoboreshwa. (Football Insider)
Brighton wako tayari kumuuza kiungo wa Ecuador Moises Caicedo lakini wanataka £85m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa akihusishwa na Chelsea na Newcastle United. (Sunday Morror)
Everton na Brighton wanavutiwa na beki wa kushoto wa Monaco, 25, Caio Henrique. (IG Esporte – kwa Kireno)
Beki wa West Ham Muingereza Craig Dawson, ambaye nusura ajiunge na Wolverhampton Wanderers msimu huu wa joto, anataka kuondoka The Hammers Januari. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 utakamilika msimu ujao wa joto. (Football Insider)
Meneja wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel anasema bado hajafanya uamuzi kuhusu ni lini atarejea kwenye uongozi baada ya kuchukua likizo kwenye mchezo huo. (Sportstar)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE