Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI (9.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI (9.10.2022)

0

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anaweza kuwa amepata mwanya wa kutimka Manchester United kuhamia Inter Miami, klabu inayomilikiwa na mchezaji mwenzake wa zamani David Beckham. (Sun)

Kipa wa Nice raia wa Denmark Kasper Schmeichel, 35, anaweza kuhama tena katika dirisha la usajili la Januari, miezi sita tu baada ya kuondoka Leicester. (L’Equipe via Leicester Mercury)

Barcelona inasaka beki wa kulia na wanamnyatia Diogo Dalot wa Manchester United, ambapo kandarasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 pale Old Trafford inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sport)

Leeds United wamekubaliana maslahi binafsi na Cody Gakpo na sasa wanafanyia kazi ada ya uhamishowanayoitaka PSV Eindhoven kwa ajili ya winga huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 23. (Mirror)

Southampton wanamfuatilia winga wa Celtic Mreno Filipe Jota, 23. (Football Insider)

Liverpool walikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa Mali, Yves Bissouma, 26, msimu wa joto kabla ya nyota huyo kujiunga na Tottenham Hotspur akitoke Brighton.(The Athletic).

Paris St-Germain wanatakata kumrejesha katika klabu hiyo huku kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, anbaye mkataba wake na Juventus unamaliza mkataba msimu ujao wa joto. (Fichajes)

Arsenal imepata pigo kubwa katika harakati zake za kumsaka nyota wa Juventus Manuel Locatelli, 24, baada ya kiungo huyo wa kati wa Italia kuamua kusalia Turin. (Football London)

Manchester United wanapanga kukutana na wakala wa Alejandro Garnacho kujadili kandarasi mpya ya winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 18. (AS via Sport Witness)

Mshambulizi wa Roma Muingereza Tammy Abraham, 25 amekataa kukataa kurejea katika klabu ya utotoni ya Chelsea katika siku zijazo. (90 Min)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here