Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO (12.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO (12.10.2022)

0

Mshambulizi wa Ufaransa Kylian Mbappe atagharimu kati ya euro 300-350m kama klabu yoyote itataka kumnunua, ingawa Paris St-Germain hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 baada ya ripoti kuibuka kwamba anataka kutimka katika dirisha la Januari. (Telegraph)

Mkataba wa mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland, 22, una kipengele cha kuuzwa kwa euro 200m ambacho kitaanza msimu wa joto 2024. Meneja Pep Guardiola aliwahi kusema mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway hakuwa na kipengele hichi kwa ajili ya “Real Madrid au timu nyingine yoyote” lakini kifungu hicho kinatumika kwa klabu yoyote nje ya Uingereza. (Athletic)

Tottenham inamfuatilia mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney wakiwa wanamtazama mara kwa mara mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Football Insider)

Chelsea wameanza mazungumzo na kiungo wa kati wa England Mason Mount, 23, kuhusu kandarasi mpya. (Standard)

Chelsea wanataka kusitisha mkataba wa wa mkopo wa kiungo wa kati wa Uswizi Denis Zakaria mwenye umri wa miaka 25 kutoka Juventus mwezi Januari, na wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya winga wake kutoka Morocco Hakim Ziyech, 29. (90min).

Beki wa kati wa Brazil Thiago Silva, 38, anasema familia yake itaamua iwapo ataongeza mkataba Chelsea, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Standard)

Juventus wanataka kumsajili mlinzi wa Manchester United Diogo Dalot huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 akitaka kuondoka Old Trafford. (Calciomercato )

Barcelona wanakusudia kumuuza beki wa kati Samuel Umtiti mwenye umri wa miaka 28 katika majira ya joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa sasa yuko kwa mkopo Lecce. (Sport)

Mshauri wa masuala ya michezo wa PSG Luis Campos aliyejiunga na klabu hiyo mwezi Juni tu, lakini anaweza kuwaacha mabingwa hao wa Ligue 1. (Le Parisien)

Sir Jim Ratcliffe anasema angeweza kuinunua Manchester United majira ya joto lakini familia ya Glazer isingeweza kumuuzia. (Financial Times, via Goal)

Nottingham Forest imewafuta kazi vigogo wawili wa usajili, George Syrianos na Andy Scott, kufuatia uchunguzi wa matumizi ya fedha ya klabu hiyo katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Telegraph)

Bosi wa Wigan Leam Richardson yuko kwenye orodh ya kuwa meneja mpya wa West Brom baada ya The Baggies kumfukuza Steve Bruce. (Football Insider)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here