Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO (5.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO (5.10.2022)

0

Aliyekuwa meneja wa Chelsea Thomas Tuchel amekataa nafasi ya kuinoa klabu ya Bayer Leverkusen iliozorota nchini kwao Ujerumani. (Sport1)

Leverkusen wanatafuta kumteua kiungo wa zamani wa Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid Xabi Alonso kuchukua nafasi ya meneja Gerardo Seoane.. (ESPN)

Mmiliki wa Nottingham Forest, Evangelos Marinakis anafikiria kumfukuza meneja Steve Cooper na baadhi ya wafanyakazi wa klabu hiyo baada ya kushindwa mara tano mfululizo kwenye Ligi ya Premia. (Mail)

Forest wanamfikiria mkufunzi wa zamani wa Liverpool, Chelsea na Newcastle Rafael Benitez kama mbadala wa Cooper, wakati mkufunzi wa zamani wa Burnley Sean Dyche pia akiwa chaguo. (Guardian)

Manchester United wanasitasita kumruhusu fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo kuondoka katika dirisha la usajili la Januari, na huenda mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 atalazimika kusubiri hadi mkataba wake uishe msimu ujao kabla ya kuondoka Old Trafford. (Mirror)

Chelsea wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 Rafael Leao. (Star)

AC Milan wanaweza kutumia mechi yao dhidi ya Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kuzungumza na The Blues kuhusu kumsajili beki wa Uingereza Trevoh Chalobah, 23 na mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 24. (Calciomercato – in Italian)

Inter Milan wanaweza kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 25, kutoka Manchester United mwezi Januari. (Fichajes – in Spanish)

Wamiliki wa Liverpool wako tayari kufadhili uhamisho wa pesa nyingi mwezi Januari ikiwa meneja wa Reds Jurgen Klopp na timu ya kuajiri ya klabu hiyo watapata mchezaji mzuri. (Football Insider)

Mkufunzi wa Liverpool Klopp anasema alitaka kumsajili Martin Odegaard wa Arsenal, 23, kwa klabu ya awali ya Borussia Dortmund lakini kiungo huyo wa Norway alichagua kujiunga na Real Madrid.. (Goal)

Arsenal wanafikiria kumpeana kiungo wa kati wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 22, katika makubaliano ya kubadilishana na kiungo wa kati wa Juventus na Italia Manuel Locatelli, 24. (Calcio Mercato Web)

Leandro Trossard, 27, amekataa kutupilia mbali uvumi unaomhusisha na kutaka kuondoka Brighton, huku Arsenal na Chelsea wakimtaka winga huyo wa Ubelgiji. (Mail)

Everton inapanga kutumia chaguo la kumbadilisha mlinzi wa Uingereza Conor Coady, 29, kwa mkopo kutoka Wolverhampton Wanderers hadi kwa uhamisho wa kudumu kwa ada inayoaminika kuwa chini ya £10m. (Times – subscription required)

Mkufunzi wa Chelsea Graham Potter anasema lengo lake ni kumfanya kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante kuwa bora tena, na kwamba hali ya kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkataba wake unakamilika msimu ujao, ni “kati ya klabu na yeye”. (Guardian)

Sevilla wamekubaliana na meneja wa zamani Jorge Sampaoli kurejea klabuni kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui kama kocha.. (ESPN)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here