Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU (24.10.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU (24.10.2022)

0

Liverpool inaongoza kampeni ya kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 17 raia wa Ujerumani Youssoufa Moukoko. (Sport, via Mail)

Arsenal imepumzisha azma yake ya kumsajili mlinzi wa Eintracht Frankfurt raia wa Ufaransa Evan Ndicka, mwenye umri wa miaka 23, baada ya kumkabidhi raia wa Brazil Gabriel Magalhaes mkataba mpya. (Express)

Itaibidi Aston Villa illipe Euro milioni 10 (£8.68m) kumsajili Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kama Meneja wake mpya. (Telegraph)

Aliyekuwa meneja wa Tottenham Tim Sherwood anasema wasiwasi kuhusu mustakabali wa meneja wa sasa Antonio Conte unamzuia mchezaji wa kiungo cha mbele Harry Kane, mwenye umri wa miaka 29, na raia wa Korea Kusini Son Heung-min, aliye na miaka 30, kusaini mikataba mipya. (Sky Sports, via Express)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic anasema Kane ni “mojawapo ya wachezaji bora duniani”. (Talksport)

Huenda Chelsea ikampatia winga raia wa Morocco Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 29, katika mkataba wa kukabidhi mchezaji na malipo kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato)

Afisa mkuu mtendaji wa Ajax Edwin van der Sar anasema ameiambia Arsenal kwamba klabu hiyo ya Uholanzi haitomuuza mlinzi wake raia wa Argentina Lisandro Martinez, wiki kadhaa kabla ajiunge na Manchester United. (Times)

Mwamba wa Leicester City Gary Lineker anasema timu hiyo ‘ilijishindia dhahabu’ kwa usajili wa msimu wa joto wa mlinzi rai awa Ubelgiji Wout Faes mwenye umri wa miaka 24 kwa £15m. (Leicestershire Live)

Huenda mlinzi wa Manchester United Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 29, akawa imara kuichezea Ufaransa katika kombe la Dunia kutokana na kuimarika kwa jeraha lake alilopata la msuli wa paja. (ESPN)

Aliyekuwa mlinzi wa Everton Jonjoe Kenny, mwenye umri wa miaka 25, anasema alikataa mkataba mpya na timu hiyo kutokana na kwamba alibidi aondoke Uingereza kuendelea na kampeni ya kujiimarisha na timu ya Hertha Berlin msimu uliopita wa joto. (Liverpool Echo)

Machache kutoka Tetesi za Jumapili

ronaldo

Beki wa kulia wa Manchester United Mreno Diogo Dalot, 23, analengwa na Real Madrid. (Mirror) Chelsea wana nia ya kutaka mnamo mwezi Januari kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Mreno Cristiano Ronaldo, 37, ambaye yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kuondoka Old Trafford. (Sunday World)

Nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane anasema ‘’wachezaji wameonyesha mchezo mbaya zaidi’’ katika klabu hiyo huku akimtetea Ronaldo kwa kukataa kuingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Tottenham Jumatano iliyopita. (Sky Sports, via Sun)

Manchester United haijapokea maombi yoyote ya kumnunua Ronaldo licha ya kumfanya apatikane kwa uhamisho wa bila malipo. (ESPN)

Mtangazaji wa TV Piers Morgan anasema Ronaldo alikataa ofa ya pauni milioni 130 ya kucheza Saudi Arabia msimu uliopita. (Mail)

Newcastle wako tayari kutumia £25m kumsajili mshambuliaji wa Brighton wa Ubelgiji Leandro Trossard, 27, Januari. (Talking Transfers, via Express) Tottenham inaweza kuwa tayari kutoa ofa ya pauni milioni 43 kumnunua beki wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 23 Alessandro Bastoni. (Inter Live, via HITC)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here