Home KITAIFA UZOEFU KUMBE UNAWABEBA MASTAA YANGA

UZOEFU KUMBE UNAWABEBA MASTAA YANGA

0

UZOEFU wa nyota wa kimataifa waliopo ndani ya kikosi cha Yanga ikiwa ni pamoja na Djuma Shaban, Yannick Bangala na Tuisila Kisinda ni sababu ya Yanga kuwa imara.

Chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, Yanga imecheza mechi 42 za ligi bila kupoteza na jana wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1Al Hilal.

 Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kuwa kila wanapokabiliana na Yanga huwa wanabadilisha mbinu kupata ushindi kutokana na uzoefu walionao.

“Hatujawa na mwendo mzuri mbele ya Yanga hii inatokana na wao kuwa na wachezaji wenye uzoefu, hata msimu uliopita pia hatukufanikiwa kushinda.

“Unaona mchezo wetu uliopita tuliamua kubadili kabisa mbinu na tulipofanya mabadiliko tulifanikiwa kwenda nao kwa kasi lakini tulikuwa tumeshafungwa, kwa mechi zijzo tunakwenda kujipanga upya,” amesema Mkwasa.

Miongoni mwa nyota wanaounda kikosi cha Yanga ni pamoja na Sure Boy.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here