Home KIMATAIFA WAWAKILISHI WA TANZANIA NA HATMA ZAO NDANI YA DAKIKA 90

WAWAKILISHI WA TANZANIA NA HATMA ZAO NDANI YA DAKIKA 90

0

LEO kwenye anga za kimataifa kwa wawakilishi wa Tanzania ni dakika90 za maamuzi kwa timu shiriki ambazo ni Azam FC, Yanga na Simba kwenye hatua ambazo wapo.

Oktoba 16, 2022 miamba yote ya soka nchini inatarajiwa kushuka uwanjani katika kutetea na kujihakikishia ushiriki wao katika hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa barani Afrika.

Azam wanawania nafasi ya kufuzu hatua ya Makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Akhdar SC, huku Azam FC akiwa na kibarua kizito baada ya kupoteza mechi ugenini kwa kichapo cha mabao 3-0.

 Mchezo wa Azam dhidi ya Al Akhdar utapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1 za usiku.

Yanga kadhalika wanatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na Al Hilal ya Sudan katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Al Hilal majira ya saa 3 usiku wa leo, Yanga anatakiwa kupata sare ya mabao 2-2 ili aweze kufuzu katika hatua ya makundi baada ya kuruhu kufungwa  1 akiwa nyumbani katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 katika  Uwanja Mkapa jijini Dar.

Simba hii leo atawakaribisha Premio de Agosto ya Angola katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu hatua hiyo ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika huku akiwa na faida ya magoli 3-1 ambayo aliyapata ugenini dhidi ya Angola.

Wote wana kazi ngumu kwenye mashindano haya yanayoandaliwa na CAF kusaka ushindi kwa kuwa mpira ni mchezo wa makosa atakayefanya makosa ataadhibiwa.

Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kimataifa

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here