Home KITAIFA WAWILI WA YANGA KUIKOSA SIMBA KESHO KWA MKAPA

WAWILI WA YANGA KUIKOSA SIMBA KESHO KWA MKAPA

0

KIUNGO mchetuaji wa Yanga, Bernard Morrison kesho ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Pia Crispin Ngushi huyu naye anatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho kwa kuwa hajawa fiti.

Sababu ya kukosekana kwenye mchezo huo ni kutokana na adhabu ambayo alipewa kutokana na kosa la kumkanyanga mchezaji wa Azam FC kwenye mchezo wa ligi walipotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wengine wapo tayari na mazoezi ya mwisho yataamua kikosi na wale ambao wataanza.

“Morrison atakosekana kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Simba kwa kuwa ana adhabu lakini wachezaji wengine wapo vizuri.

“Sure Boy yeye alikuwa anaumwa lakini amepona hivyo kuanza kwake pia itategemea mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Simba,” amesema Nabi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here