Home KITAIFA WAZAWA KWENYE VITA YA LEO UWANJA WA MAJALIWA

WAZAWA KWENYE VITA YA LEO UWANJA WA MAJALIWA

0

MATHEO Anthony, mzawa anayekipiga ndani ya KMC akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi ndani ya KMC kwa Septemba anatarajiwa kukutana na staa namba moja wa Namungo Relliats Lusajo.

Lusajo yeye ana tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti ndani ya ligi na ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao matano msimu huu wa 2022/23.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa na kila timu zimeweka wazi kuwa zinahitaji pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba wakati KMC ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, Matheo alipachika bao moja na kumfanya afikishe mabao manne ndani ya ligi.

Lusajo yeye mbele ya Coastal Union alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalti na kumfanya afikishe mabao matano.

Hivyo ni vita ya wazawa kwenye kuongeza idadi ya mabao na kuipa pointi tatu timu yake husika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here