Home KITAIFA YANGA PRINCESS NAO WAZIDI KUWA WANONO, WASAINI DILI LA MAMILIONI

YANGA PRINCESS NAO WAZIDI KUWA WANONO, WASAINI DILI LA MAMILIONI

0

Timu ya Yanga Princess imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Watercom yenye kinywaji cha Jembe Energy, mkataba ambao Kampuni hiyo itatoa kiasi cha shilingi milioni 120 sawa na shilingi milioni 10 kila mwezi ambao utaenda sambamba na kutoa lita 1500 za maji kila mwezi kwa ajili ya timu hiyo.

Akiongea katika Mkutano na waandishi wa Habari, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema miongoni mwa vipaumbele vya timu yetu hivi sasa ni kuhakikisha inapata pato kubwa ili kuendana na kasi ya matumizi na kutengeneza timu bora:

“Huu ni muendelezo wa ajenda yangu kubwa ya kuimarisha timu kiuchumi, na kwa kupitia mkataba huu tunaendelea kuimarisha hali yetu ya kiuchumi ili kuwa imara zaidi.

“Kwa miaka mingi vilabu vyetu vimekuwa vikikumbana na adha mbalimbali za kiuchumi na hii inatokana na kukosekana mikakati imara ya kuwashawishi wadhamini. Unapokuwa na uongozi imara inasaidia hata washirika wengine kuja kuwaunga mkono. Unapokuwa na timu imara inavutia wadau wengi kuja.

Je mkataba wetu una thamani gani?

“Mkataba wetu una thamani ya Tsh milioni 120 sawa na milion 10 kwa mwezi. Vile vile watercom watatoa lita 1500 kwa klabu yetu kila mwezi” Rais Hersi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Andre Mtine amesema: “Leo ni siku muhimu sana kwetu kwenye maendeleo ya mpira. Ninajivunia kuona nasaini mkataba mpya kwa niaba ya Klabu. Hii ni hatua kubwa sana na inaonesha kwa jinsi gani klabu hii imejipanga kuboresha masuala ya kiuchumi.”

Kwa upande wa Mohamed Salim, Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Watercom nae amesema: “Timu ya Yanga Princess ni timu kubwa ambayo ina malengo ya kuweka historia kubwa kama ambavyo ipo Yanga SC ambayo inahistoria ya kipekee. Ni heshima kubwa kwetu kupata fursa hii ya kufanya nao kazi tena.

“Mkataba wetu huu wa mwaka mmoja hatuna wasiwasi na tuna imani kubwa matunda yataonekana kwa pande zote. Tutashirikiana na Yanga Princess kama wadhamini na washirika katika kutoa huduma mbalimbali kupitia vinywaji vyetu”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here