Home KITAIFA YANGA WABANISHA UGUMU KUWAKABILI AL HILAL

YANGA WABANISHA UGUMU KUWAKABILI AL HILAL

0

ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Oktoba 16,2022 baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 1-1 Al Hilal.

Alfajiri ya leo Oktoba 15,2022 kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kimekwea pipa kuelekea Sudan kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.

Kamwe amesema kuwa wanatambua mchezo wao utakuwa mgumu lakini wapo tayari ili kupata matokeo chanya.

“Tunajua kwamba mchezo wetu utakuwa mgumu na kila mchezaji anajua hilo lakini tupo tayari na tutaimani tutafanya vizuri.

“Kikubwa kwa Watanzania kuendelea kutuombea ili tuweze kupata matokeo chanya wakati wetu wa kupeperusha bendera ya Tanzania ni sasa tupo tayari mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Dickson Job, Aboutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto, Shaban Djuma, Fiston Mayele na Zawad Mauya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here