Home KITAIFA YANGA WAPAGAWA NA WALIVYOPOKELEWA SUDAN….ALLY KAMWE ASHINDWA KUJIZUIA

YANGA WAPAGAWA NA WALIVYOPOKELEWA SUDAN….ALLY KAMWE ASHINDWA KUJIZUIA

0

Wakati Al Hilal ikiwa inasifika kwa mashabiki wake kuwa na vurugu dhidi ya wapinzani wanaokwenda kucheza nchini humo hali imekuwa tofauti kwa wawakilishi wa Tanzania, Timu ya Yanga.

Yanga ambao walisafiri jana kwenda Sudan kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa marudiano kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, walikua na tahadhari zote dhidi ya kila aina ya figisu lakini hawajakutana na madhila ya aina yoyote katika mapokezi yao.

“Tumepokelewa vizuri sana. Hakuna mizengwe. Hakuna Fujo. Ule Wema alioutenda Rais wetu @caamil_88 umeonekana matunda yake” amesema Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe

Yanga inashuka dimbani leo Jumapili Oktoba 16, majira ya saa 3:00 usiku huku ushindi wa aina yoyote kwa Yanga utamuhakikishia kufuzu ama sare ya kuanzia magoli mawili na kuendelea.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here