Home KIMATAIFA YANGA YATOSHANA NGUVU NA AL HILAL KWA MKAPA

YANGA YATOSHANA NGUVU NA AL HILAL KWA MKAPA

0

DAKIKA 90 zimekamilika, Uwanja wa Mkapa kwa timu zote mbili kutoshana nguvu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ubao umesoma Yanga 1-1 Al Hilal, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Pili, mchezo ujao Yanga wanakibarua cha kusaka mabao zaidi ya mawili.

Watupiaji ni Fiston Mayele dakika ya 50 na kwa Al Hilal ni dakika ya 67 kwa Mohamed Youseif dakika ya 64.

Mabao yote yamefungwa kipindi cha pili ambapo kipindi cha kwanza hakuna timu ambayo ilifanikiwa kupata bao.

Kiungo Bernard Morrison ni miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye kazi kubwa mbele ya Al Hilal kwenye mchezo wa leo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here