Home KITAIFA YANGA YATUMA WAWILI SUDAN

YANGA YATUMA WAWILI SUDAN

0

Viongozi wa Yanga wanajipanga kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal na jana Jumatatu wameondoka vigogo wawili kwenda Sudan tayari kwa maandalizi ya awali kabla ya timu hiyo kusafiri baadaye wiki hii.

Yanga inawatanguliza mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh pamoja na kigogo mwingine wa Kamati ya Mashindano ya Klabu ili kuweka mambo sawa kwa maandalizi kabla ya mchezo huo ambao timu hiyo inahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare inayozidi bao moja ili irejee rekodi ya mwaka 1998 ilipocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiongea na Mwanaspoti, kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi alisema Yanga haitakwenda kinyonge jijini humo na wala hawatakwenda na mbinu za kujilinda katika mchezo huo ambao utapigwa Jumapili.

“Kuna sehemu tulifanya makosa sana ya kutotumia nafasi ambazo tulizitengeneza, tulicheza vizuri sana kipindi cha kwanza hasa dakika 55 za kwanza, tuliporuhusu goli hatukuonyesha ukomavu, tulinyon g’onyea sana,” alisema Nabi na kuongeza;

“Tunajua makosa yetu pia tunafahamu mashabiki wetu wameumia sana, huu ndio mchezo wa soka, hatujakata tamaa na wala hatutakwenda kurudiana nao tukiwa na akili ya kujilinda. Tutakwenda kuipigania Yanga, hii ni vita ya soka bado haijaisha tutazungumza na wachezaji kubadilisha muelekeo wa akili yao.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here