Home KITAIFA ZIMBWE: TUTACHEZA KWA USHIRIKIANO, MASHABIKI WAJITOKEZE

ZIMBWE: TUTACHEZA KWA USHIRIKIANO, MASHABIKI WAJITOKEZE

0

MOHAMED Hussein Zimbwe Jr, nahodha wa Simba amesema kuwa hawataangalia mchezaji mmoja kwenye kukaba bali kila mchezaji atatimiza majukumu yake kwa ushirikiano.

Akijibu swali la mwandishi wa habari alipoulizwa kuhusu safu ya ulinzi kumtolea macho mshambuliaji Fiston Mayele wanapokutana amesema kuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana.

Kesho Oktoba 23,2022 Simba inatarajiwa kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni Kariakoo Dabi.

Zimbwe amesema wanatambua uimara wa wapinzani wao na mchezo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kupata ushindi.

“Uimara wao na tunawaheshimu lakini hatutaingia uwanjani kumkaba mchezaji mmoja hapana, tutacheza tukiwa ni timu na tutashirikiana kutafuta ushindi mashabiki wawe pamoja nasi,” amesema Zimbwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here