Home KITAIFA AZAM FC KUKIPIGA NA DODOMA JIJI, BURE KUWAONA MASTAA

AZAM FC KUKIPIGA NA DODOMA JIJI, BURE KUWAONA MASTAA

0

KIKOSI cha Azam FC leo Novemba 9 kina kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Timu hiyo iliyo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala imekuwa kwenye mwendo mzuri baada ya kushinda mechi mbili za ligi mfululizo kwa kuanza na Simba kisha Ihefu na ushindi wao ni mwendo wa bao mojamoja.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amebainisha kuwa mchezo wa leo ni muhimu kupata ushindi licha ya ugumu ambao watakutana nao.

Aidha hakutakuwa na kiingilio kwenye mchezo wa leo amesema Ibwe hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani.

“Mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji tunaamini kwamba utakuwa mgumu kwani wapinzani wetu wanahitaji ushindi, kikubwa ambacho tunahitaji kuona ni kwamba tunapata pointi tatu.

“Kila mmoja anaona namna ushindani ulivyo mgumu nasi pia tunazidi kupambana kwani wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mechi zetu.

“Hakutakuwa na kiingilio kwenye mchezo wetu dhidi ya Dodoma, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna gani tunaedeleza kutoa burudani,” amesema.

Miongoni mwa mastaa wa Azam FC ambao walikuwa kwenye mazoezi ya mwisho ni pamoja Ibrahim Ajibu, Idd Nado,Ayoub Lyanga, Sospeter Bajana.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here