Home KITAIFA AZAM FC SAFU YAO YA USHAMBULIAJI INAZIDI KUIMARIKA

AZAM FC SAFU YAO YA USHAMBULIAJI INAZIDI KUIMARIKA

0

KALI Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa washambuliaji wake wote wanazidi kuwa imara kwenye kila mchezo ambao wanacheza jamb linalowapa matokeo chanya.

Staa Prince Dube wanamuita Mwana wa Mfalme amekuwa kwenye kasi nzuri katika mechi mbili za ligi za hivi karibuni akifunga mabao yaliyoipa pointi tatu muhimu timu hiyo.

Aliwatungua Simba na Ihefu kwa mguu wa kulia wakati wakisepa na pointi sita kwenye ligi.

Ongala amesema:”Kila mchezaji kwenye safu ya ushambuliaji anatimiza majukumu yake na ni jambo la furaha kwetu kupata matokeo, tunaona maandeleo kwenye kila hatua,”.

Mchezo ujao wa ligi wa Azam FC ni dhidi ya Dodoma Jiji unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Novemba 9,2022.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here