Home KITAIFA AZAM FC YAWEKA REKODI YA KIBABE MSIMU HUU

AZAM FC YAWEKA REKODI YA KIBABE MSIMU HUU

0

Azam FC imeandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwenye msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC, kushinda mechi tano mfululizo za ligi hiyo.

Mechi hizo, imeshinda ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Kali Ongala na wasaidizi wake, Agrey Morisambros, @danicadena13, @johnyonatas, @dr.moadh_hiraoui.

Ilianza kwa kuichapa Simba bao 1-0, kabla ya kuinyuka Ihefu (1-0), ikaigagadua Dodoma Jiji (2-1), ikailaza Mtibwa Sugar (4-3) kabla Jumanne iliyopita kuinyoa Ruvu Shooting (1-0).

Klabu hiyo bora ya viwango kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 26 sawa na Yanga iliyo kileleni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here