Home KITAIFA AZAM HAWATANII KWA FEI TOTO

AZAM HAWATANII KWA FEI TOTO

0

Ikiwa imesalia takribani miezi miwili dirisha Dogo la usajili la mwezi Januari kufunguliwa, inasemekana Bosi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa ameanza kufanya michakato ya kuboresha kikosi cha Azam na rada yake imetua kwa Nyota wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto).

Inasemekana Fei Toto na Bakhresa wapo mezani kujadili matakwa ya mchezaji huyo na endapo wataafikiana basi kiungo huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini akiwa na kikosi cha Yanga huenda akamwaga wino kuwatumikia matajiri wa Jiji la Dar es Salaam.

Fei Toto ana Mkataba na mabingwa hao watetezi hadi mwaka 2024 na inasemeka kuwa kuvunja mkataba wake anahitajika kuwalipa Yanga Tsh. milioni 100 na mshahara wake wa miezi mitatu.

Klabu ya Yanga SC imeeleza kuwa, watu waache kuota, Feisal Salum hauzwi kwa gharama yoyote.

Msemaji wa klabu hiyo Alli Kamwe alipoulizwa kuhusu tetesi zilizozagaa leo zikianzishwa na kituo cha Wasafi FM kuwa Azam FC imeandaa kitita ili kumnunua Feisal dirisha dogo, Alli Kamwe amesema;

“Feisal kwenda Azam ?! Labda atakwenda kwenye boti ya AZAM MARINE wakati akielekea nyumbani kwao Zanzibar. Hakuna klabu inayoweza kumnunua Feisal Salum kutoka Yanga hapa Tanzania labda nje,” amesema Ally Kamwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here