Home KITAIFA BANGALA. AZIZ KI TAYARI KUIKABILI MBEYA CITY

BANGALA. AZIZ KI TAYARI KUIKABILI MBEYA CITY

0

CEDRICK Kaze kocha msaidizi wa Yanga ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City kuna baadhi ya wachezaji ambao watarejea kutokana na kuwa na adhabu.

Kesho Yanga ambao wamecheza mechi 48 za ligi bila kufungwa wana kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Mbeya City mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Kaze amesema:”Aziz KI, Yannick Bangala hawa walikosekana kwenye mechi zilizopita lakini kwa sasa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City na tunaweza tukawatumia.

“Tumekuwa na rekodi nzuri ya kutofungwa lakini haujawaambia wachezaji kwamba tunahitaji kufanya jambo gani lingine zaidi ya kupata ushindi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza.

“Mbeya City tunawaheshimu ni timu imara na imekuwa na matokeo mazuri, hatuangalii imetoka kucheza na nani lakini tunachojua ni kwamba imekuwa na matokeo mazuri,” Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here