Home KIMATAIFA BECKHAM NA INTER YAKE WAMKOMALIA MESSI

BECKHAM NA INTER YAKE WAMKOMALIA MESSI

0

Inter Miami imeongeza nguvu ya kutaka kumsajili Lionel Messi baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa kimataifa wa Argentine mwenye miaka 35, anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake ndani ya Paris Saint-Germain.

Wakati miamba hiyo ya Ligue 1 ikitaka kumbakiza, gazeti la The Athletic kwa mshangao liliandika jana kuwa klabu inayomilikiwa na David Beckham ya Ligi ya Marekani, MLS inataka kupambana kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa zamani wa Barcelona.

Mazungumzo yamepangwa kuanza tena baada ya Messi kutoka Qatar, huku Inter Miami ikiwa katika nafasi nzuri ya kumnasa mbele ya mkataba mpya wa kubaki PSG au kurudi Barcelona.

Ndugu wawili, Jorge na Jose Mas ambao pia wanaimiliki Inter pamoja na Beckham wanaongoza mazungumzo hayo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here