Home KITAIFA BEKI WA KAZI YANGA KUWAKOSA WAARABU LEO

BEKI WA KAZI YANGA KUWAKOSA WAARABU LEO

0
KWENYE mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Africain v Yanga mwamba Djuma Shaban hatakuwa sehemu ya kikosi.Sababu kubwa ya nyota huyo kuwekwa kando kuwakabili Waarabu wa Tunisia ni kutokuwa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa kwanza.

Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi nchini Tunisia baada ya ule mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 0-0 Club Africain.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kwamba wanatambua utakuwa ni mchezo mgumu lakini wapo tayari kwaajili ya ushindani.

“Wachezaji ambao tupo nao kwenye msafara ni wale ambao wapo tayari tunaamini tutafanya kazi kubwa kutafuta ushindi,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Olympique Hamadi Agrebi saa 2:00 usiku.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here