Home KITAIFA DAKTARI AFICHUA KILICHOMKUMBA MWAMNYETO JUZI

DAKTARI AFICHUA KILICHOMKUMBA MWAMNYETO JUZI

0

Naodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto anaendelea vizuri kwa sasa baada ya juzi Novemba 22, 2022 kushindwa kumaliza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kwa kupata majeraha.

Akizungumza na Yanga Media, Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema Mwamnyeto alipata shida kidogo ya upumuaji baada ya misuli ya upumuaji kuchoka.

“Hali Kama hii huwatokea wanamichezo kwa sababu Kama kucheza kwa kutumia nguvu sana, uchovu wa safari hii husababisha misuli ya upumuaji kuchoka na kumpa shida wakati wa kupumua.

“Kwa sababu mchezaji wakati huo hutumia muda mwingi sana kupumua kwa nguvu. Tumempatia matibabu na sasa naweza kusema Mwamnyeto yupo fiti kabisa,” amesema Etutu.

Kwa upande wa naodha Mwamnyeto amesema anamshukuru Mungu kwanza kwa kumjalia afya njema hadi sasa pia anawashukuru jopo la madaktari wa Yanga kwa kumpa matibabu mazuri.

Mwamnyeto anasema; “Wakati wa mchezo unaendelea mbavu zilinibana sana na kushindwa kupumua vizuri ndipo nikaomba msaada kwa benchi la ufundi wanifanyie mabadiliko ila kwa sasa namshukukuru sana Mungu kwa kunifanyia wepesi wa kunijalia afya njema,” amesema Mwamnyeto.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here