Home KITAIFA HALI YAZIDI KUWA MBAYA KWA PETER BANDA, SIMBA WATOA TAMKO HILI RASMI

HALI YAZIDI KUWA MBAYA KWA PETER BANDA, SIMBA WATOA TAMKO HILI RASMI

0

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema Kiungo Mshambuliaji Peter Banda atakuwa nje ya Uwanja kwa Majuma manne ama zaidi.

Kiungo huyo kutoka nchini Malawi aliiokoa Simba SC kwenye mchezo wa jana Jumatano (Novemba 09), kwa kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Singida Big Stars iliyotangulia kufunga kupitia kwa Deus Kaseke.

Akizungumza baada ya kikosi cha Simba SC kurejea jijini Dar es salaam mapema leo Alhamis (Novemba 10), Ahmed amesema Banda alilazimika kukimbizwa hospitali alipopata majeraha na imebainika aliumizwa eneo la kifundo cha mguu.

“Banda atakosekana kwa muda wa majuma manne hivi ama zaidi, maana alipelekwa hospitali jana ile ile baada ya kupata jeraha, imebainika ameumia eneo la kifundo cha mguu.”

“Akiwa hapa Dar es salaama atafanyiwa vipimo tena ili kujiridhisha zaidi ukubwa wa jeraha lake, tufahamu kwa undani namna ya kumsaidia kimatibabu,” amesema Ahmed Ally.

Kikosi cha Simba SC baada ya kurejea jijini Dar es salaam moja kwa moja kimekwenda kambini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi kuu dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi (Novemba 12).

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here