Nyota 10 wa timu ya taifa ya soka kwa watu wenye ulemavu (Tembo Warriors) wamesajiliwa kucheza soka la kulipwa nchini Uturuki.
Wachezaji hao ni Alfan Kyanga, Juma kidevu, Habibu Likoike na Shedrack Hebron waliosajiliwa kwenye klabu ya Sisli Yeditepe.
Wengine ni Abdulkarim Amiri na Salimu Bakari waliosajiliwa na klabu ya Keysari na Ramadhan Chomelo aliyejiunga na klabu ya Konya.
Wakati Frank Ngailo akiwa kwenye klabu ya Izmir BBSK na Mudrick Azzan na Richard Swai wakiwa kwenye klabu ya Mersin.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE