Home KITAIFA HESABU ZA YANGA KIMATAIFA NI KUANZA NA USHINDI

HESABU ZA YANGA KIMATAIFA NI KUANZA NA USHINDI

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa mpango kazi namba moja ni kuanza kupata ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Kesho Novemba 2, Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa mtoano kuwania kufuzu hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa kisha ule wa pili Yanga itakuwa ugenini nchini Tunisia kukamilisha kete ya pili.

“Maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji anajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo na benchi la ufundi linahitaji kuona tunapata kile ambacho tunastahili.

“Kuna kazi kubwa inahitajika kufanyikakwa wachezaji ili kupata matokeo kwani kwenye hatua hizi kila timu inaigia uwanjani ikiwa inajiamini na malengo ni kupata ushindi,”.

Nabi anafanya kazi kwa ushirikiano na msaidizi wake Cedrick Kaze.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here