Home KITAIFA HUYU HAPA MKALI WA KUTUPIA BONGO

HUYU HAPA MKALI WA KUTUPIA BONGO

0

MZAWA namba moja kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara ni Sixtus Sabilo anayekipiga ndani ya Mbeya City inayotumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani.

Kibindoni katupia mabao 7 ambapo mchezo uliopita mbele ya Coastal Union kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 alitupia mabao yote mawili kimiani.

Ilikuwa dakika ya 39 na dakika ya 80 kwa mkwaju wa penalti wakati wakigawana pointi mojamoja.

Mzawa huyo kwenye kabati ana tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba ambapo kwa upande wa kocha tuzo hiyo ipo mikononi mwa Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga.

Ikumbukwe kwamba anayemfuata Sabilo kwenye kasi ya utupiaji ni mzawa mwingine Relliats Lusajo yupo zake ndani ya Namungo.

Nyota huyo katupia mabao 6 kibindoni naye ni miongoni mwa walioitungua Coastal Union kwa penalti ambapo alifikisha bao lake la tano walipokutana na timu hiyo.

Sabilo amesema kuwa kikubwa ibada pamoja na jitihada bila kuchoka.

“Kwenye kila jambo ambalo ninafanya ninaanza na Mungu pamoja na jitihada ndani ya uwanja na kushirikiana na wachezaji wenzangu.

“Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi nasi tunapambana kufanya vizuri na kupata matokeo chanya”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here