Home KITAIFA IHEFU WATAJA WALIPOKWAMIA

IHEFU WATAJA WALIPOKWAMIA

0

JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa mpango kazi ulivurugika baada ya timu hiyo kufungwa bao kipindi cha pili.

Katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Novemba 12,Uwanja wa Mkapa, Ihefu ilifanikiwa kutoruhusu bao ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili walikwama kulinda na kufunga na kuruhusu bao la Pape Sakho dakika ya 63 kwa shuti lililomshinda mlinda mlango wa Ihefu.

“Ilikuwa ni kazi kubwa kwetu kutafuta ushindi lakini mpango kipindi cha pili ulivurugika baada ya kufungwa bao lakini wachezaji walicheza kwa umakini na kushindwa kupata bao.

“Kwa mechi zijazo tutafanyia kazi ili kuwa imara zaidi inawezekana na kupoteza kwenye mechi zetu zilizopita sio jambo zuri,” amesema.

Kichapo hicho kinaifanya Ihefu kubaki na pointi zake5 nafasi ya 16 huku Simba ikifikisha pointi 21 nafasi ya pili.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here