Home KITAIFA INJINIA HERSI: MASHABIKI YANGA WANATUKOSEA SANA

INJINIA HERSI: MASHABIKI YANGA WANATUKOSEA SANA

0

Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Saidi amesema pamoja na timu kukosa ushindi dhidi ya Club African katika mchezo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika lakini bado haijakata tamaa.

Hersi amesema wachezaji pamoja na benchi la ufundi walitumia kila mbinu ndani ya uwanja lakini ilishindikana na kwamba bado wana matumaini ya kufanya vizuri katika mechi ya marudiano.

Nimeona maoni mengi ya mashabiki wetu wakitupia lawama benchi la ufundi, wachezaji na hata viongozi, wanakosea hiyo ni kuwavumja nguvu wachezaji. Wachezaji na benchi la ufundi walipambana, naamini haikuwa bahati kwetu ila tunazo dakika 90 nyingine za kujiuliza

Alisema Hersi

Amesema kinachofafanyika hivi sasa ni kuiandaa timu kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili kutimiza lengo la kucheza hatua ya makundi ingawa amekiri kuwa mchezo utakuwa mgumu.

Club Africain itaikaribisha Yanga katika mchezo wa marudiano Tunisia Novemba 9, 2022.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here