Home KITAIFA ISHU YA MATOLA KUSEPA SIMBA UONGOZI WABARIKI

ISHU YA MATOLA KUSEPA SIMBA UONGOZI WABARIKI

0

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa umetoa baraka zote kwa kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola kuondoka.

Matola anatarajiwa kuanza masomo ya masuala ya ukocha ambapo anatafuta Leseni A itakayompa fursa ya kuwa kocha mkuu kwenye timu yoyote.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa ndani ya timu na hawana tatizo na Matola.

“Hakuna tatizo lolote ambalo lipo na tunajua kwamba Matola amepata fursa ya kwenda kusoma hili ni jambo jema na zuri kabisa.

“Uongozi umebariki suala la yeye kwenda kusoma na kuhusu kurejea kwenye nafasi hiyo ni mpaka pale ambapo atakamilisha masomo kwani kwa sasa bado ni mapema kuzungumzia hilo,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here