Home KITAIFA KISA KUPEWA UNAHODHA MAYELE AANDIKA HISTORIA YANGA

KISA KUPEWA UNAHODHA MAYELE AANDIKA HISTORIA YANGA

0

FISTON Kalala Mayele ameanza kucheza kwenye Ligi ya ushindani mwaka 2013 nchini Congo.

Alianza kwenye klabu ya mtaani kwao ya Jsl ya Lkasi ya Lubumbushi, kisha akahamia AS SIMBA ya mjini Kolwezi kisha baada akajiunga AS Vita Club.

Ni zaidi ya mechi 200 ukijumlisha na zile alizocheza akiwa na jezi ya Yanga msimu uliopita, lakini jambo moja ambalo huwezi kuamini, Mayele hakuwahi kuvaa kitambaa cha unahodha wa timu yoyote hata kwa dakika moja.

Mara yake ya kwanza kuwa nahodha uwanjani ni kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa katika uwanja wa CCM Liti, mkoani Singida. Historia imeandikwa.

Na sio historia ya kuvaa kitambaa cha unahodha peke yake, historia kubwa ni Mayele kufunga bao akiwa na kitambaa cha unahodha kwenye mkono wake.

Akizungumza na YANGA MEDIA baada ya mchezo huo, Mayele amesema anawashukuru sana wachezaji wenzake kumsaidia kufunga bao la pili kwenye mchezo huo kwani imekuwa mara yake ya kwanza katika historia yake ya soka.

“Hii ni mara ya kwanza katika historia yangu ya mpira kuvaa kitambaa cha unahodha. Nimefurahi sana katika kipindi kifupi nilichokuwa nahodha uwanjani niliweza pia kufunga bao.

“Nawapongeza sana wachezaji wenzangu kwa ushindi huu na mchango wao hadi kufunga mabao mawili kwenye uwanja wa Liti,” alisema Mayele

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here