Home KITAIFA KOCHA MPYA WA VIUNGO SIMBA HUYU HAPA, ’PROFAILI’ YAKE SIO LA KITOTO

KOCHA MPYA WA VIUNGO SIMBA HUYU HAPA, ’PROFAILI’ YAKE SIO LA KITOTO

0

Uongozi wa Simba SC umepanga kumtangaza Kocha wa Viungo wakati wowote kuanzia sasa, ili kuimarisha viwango vya wachezaji ambao wana jukumu la kuipa matokeo klabu hiyo ya Msimbazi.

Kwa siku za karibuni Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wamekua wakitoa malalamiko juu ya wachezaji wa timu hiyo kutokuwa na utimamu wa miili, wakidai hali hiyo inasababishwa na kutokuwepo kwa Kocha wa Viungo.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema wakati wowote kuanzia sasa watamtangaza Kocha Mpya wa Viungo ambaye ana viwango vya juu.

Ahmed amesema wapo katika mazungumzo na Kocha huyo ambaye jina lake wamelificha kwanza, lakini wakikamilisha kila kitu watakiweka hadharani.

“Wakati wowote kuanzia juma hili tutakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kwa ajili yakumtangaza Kocha wa Viungo atakayeungana na Benchi letu na Ufundi ambalo linaongozwa na Kaimu Kocha Mkuu Juma Mgunda.”

“Niwatoe wasiwasi wanasimba, wakati wowote kuanzia sasa Simba SC itakua na Kocha wa Viungo mwenye viwango vinavyostahili kuwa kwenye klabu yetu, ili kuhakikisha wachezaji wetu wanakuwa na utimamu wa kutosha kupambania mataji msimu huu.” amesema Ahmed Ally.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here