Home KIMATAIFA KUELEKEA QATAR: SENEGAL KUTUMIA WAGANGA WA KIENYEJI KUMTIBU SADIO MANE

KUELEKEA QATAR: SENEGAL KUTUMIA WAGANGA WA KIENYEJI KUMTIBU SADIO MANE

0

Katibu Mkuu wa FIFA Msenegal Fatma Samoura, amesema kuwa Senegal itatumia Waganga wa kienyeji ili kuhakikisha Sadio Mané (30) anashiriki katika fainali za Kombe la Dunia 2022.

Mané alipata jeraha la tendon wakati wa mchezo wa Bayern Munich dhidi ya Werder Bremen mapema wiki hii ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa mwezi mmoja.

Hata hivyo iliripotiwa kuwa Mané anaweza kushiriki Kombe la Dunia huku ikielezwa kuwa kocha wa Senegal Aliou Cissé anatarajia kumjumuisha katika kikosi chake atakachokitangaza siku ya Ijumaa.

“Tutatumia waganga,” amesema Somoura

Alipoulizwa juu ya ufanisi wa waganga alijibu:-

“Sijui (kama zinafaa) lakini katika hali hii, tutazitumia hivyo hivyo. Tunatumaini miujiza. Lazima awepo Qatar

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here