Home KITAIFA MATAIFA YALIYOIPELEKA YANGA KIMATAIFA

MATAIFA YALIYOIPELEKA YANGA KIMATAIFA

0

MATAIFA matatu yalifanya kazi kubwa kuipaisha Yanga kimataifa na kuipeleka kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni kupitia bao pekee la ushindi la Aziz Ki raia wa Burkina Faso ambaye alifunga bao hilo dakika ya 79 akitumia pasi ya Fiston Mayele raia wa DR Congo.

Ikumbukwe kuwa kabla ya bao kupatikana lilipita kwenye miguu ya wazawa wawili ambao ni Farid Mussa aliyemmegea pande Salim Aboubhakari aliyetoa pasi kwa Mayele.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa kila mchezaji anatimiza majukumu yake kwa wakati kwa ajili ya ushindi.

“Wachezaji wote wanatimiza majukumu ambayo wanapewa na ushirikiano ni jambo kubwa linalofanyika kwa kila mchezaji hivyo ushindi kwetu ni jambo linalotupa furaha,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here