Home KITAIFA MCHEZO WA COASTAL UNION V DODOMA JIJI KUPANGIWA TAREHE

MCHEZO WA COASTAL UNION V DODOMA JIJI KUPANGIWA TAREHE

0

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Coastal Union v Dodoma Jiji kwa sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya ile ya awali kushindikana.

Novemba 5,2022 mchezo huo ulipaswa kuchezwa kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

Ni Uwanja wa Mkakwani Tanga mchezo huo ulipaswa kuchezwa ambapo timu zote zilikuwa zimefanya maadalizi kutoa burudani kwa mashabiki zao.

Taarifa kutoka Dodoma Jiji zimeeleza kuwa walikuwa wamekamilisha maandalizi kwa ajili ya mchezo huo lakini baada ya kupewa taarifa kuhusu ratiba kubadilika wamefanya maamuzi mengine.

“Awali mchezo ulipaswa kuchezwa Jumamosi lakini tumepewa taarifa kwamba hautachezwa ni mpaka tutakapopewa taarifa mpya kuhusu mchezo wetu kupangiwa tarehe,” .

Kwa sasa Dodoma Jiji wanajiandaa kwa mchezo ujao wa ligi dhidi ya Azam FC  unaotarajiwa kuchezwa Novemba 9,uwanja wa Azam Complex..

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here