Home KITAIFA MGUNDA APANGA ‘KUISHINDILIA’ IHEFU KESHO

MGUNDA APANGA ‘KUISHINDILIA’ IHEFU KESHO

0

Baada ya sare ya bao 1-1 waliyoipata kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Singida Big Stars, Kocha wa Simba, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa mechi yao ijayo dhidi ya Ihefu FC itakuwa ni ya kurekebisha makosa ya mechi iliyopita.

Kesho Jumamosi Simba watashuka dimbani kucheza na Ihefu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mgunda alisema kuna kila sababu ya wao kupata ushindi kwenye mechi yao ijayo kwa kuwa tayari wamepoteza alama mbili kwenye mechi iliyopita na wanatakiwa kufanya kila kinachowezekana ili kushinda dhidi ya Ihefu.

Mgunda alisema: “Tumefanya makosa kwenye mechi iliyopita na tunakubali kwa sababu imeshatokea na hakuna namna ya kuweza kuubadilisha ukweli. Lakini tunatakiwa kurekebisha hayo kwenye mchezo ujao.

“Tukubali kuwa kuna makosa yalifanyika kwenye upande wetu na sisi kama benchi la ufundi tunakwenda kukaa chini na kuyarekebisha haraka kabla ya kwenda uwanjani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here