Home KITAIFA MGUNDA:WAKATI WA KIBU UNAKUJA

MGUNDA:WAKATI WA KIBU UNAKUJA

0

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wakati wa kufunga kwa mshambuliaji wake Kibu Dennis unakuja.

Nyota huyo msimu wa 2021/22 alikuwa mfungaji bora ndani ya kikosi cha Simba alipotupia mabao 8 kibindoni.

Msimu huu hajafunga bao zaidi ya kutoa pasi moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alipompa mshikaji wake Jonas Mkude.

Mgunda amesema:”Kwa sasa kila mchezaji anatimiza majukumu yake ndani ya timu na nina amini kwamba kwenye upande wa ufungaji tutakuwa vizuri pia.

“Kuhusu Kibu mwanangu wakati wake unakuja na atafunga hivyo ni suala la kusubiri kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here