Home KIMATAIFA MKONGWE PIQUE AWAAGA BARCELONA

MKONGWE PIQUE AWAAGA BARCELONA

0

MKONGWE wa kazi ndani ya uwanja alikwama kuzuia machozi yasimtoke wakati akiwaaga mashabiki wake.

Alizungumza mengi ikiwa ni pamoja na maneno haya:- “Nitawakumbuka na nina amini nitarudi kwa wakati mwingine lakini sitakuwa ni mchezaji wakati nitakaporudi,” ni Gerard Pique amebainisha hayo ndani ya Uwanja wa Nou Camp.

Ilikuwa ni Novemba 5,2022 wajati ubao ukisoma Barcelona 2-0 Almeria nyota huyo alipewa muda wa kuwaaga mashabiki waliojitokeza ambao walionyesha utulivu mkubwa.

Kocha Mkuu wa Barcelona, Xavi Hernandez amebainisha kuwa mechi ya mwisho kwa beki huyo wa kazi itakuwa dhidi ya Osasuana inayotarajiwa kuchezwa Jumanne.

Ikumbukwe kwamba Alhamisi ya wiki hii beki huyo alitangaza kustaafu soka na kusepa Barcelona licha ya kwamba ana mkataba na timu hiyo.

Kwenye mchezo huo ni mabao ya Ousmane Dembele dakika ya 48 na Frenkie de Jong dakika 62.

Barcelona ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 34 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 11, sare moja na kichapo mechi moja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here