Home KITAIFA NABI: HUU NI MPIRA..AZIZI KI NI ZAIDI YA FEI TOTO UWANJANI

NABI: HUU NI MPIRA..AZIZI KI NI ZAIDI YA FEI TOTO UWANJANI

0

Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Stephen Aziz Ki, anazidi kuimarika kutokana na uwezo ambao ameuonesha kwenye Michezo iliyowakabili msimu huu 2022/23.

Ndani ya Ligi Kuu Tanzana Bara, Kiungo huyo ameshacheza michezo saba kati ya nane, akitumia dakika 468, ametupia mabao mawili, ana pasi moja ya bao.

Kocha Nabi amesema kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri katika kikosi chake na ametoa mchango mkubwa katika ushindi walioupata kwenye michezo ya Ligi Kuu.

“Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji wazuri ambao wanafanya kazi kubwa kwa ushirikiano, nasikia mashabiki wanalalamika kuhusu nafasi anayocheza, muda mwingine wanasema ninamchezesha nafasi ya Feisal Salum, hapana, huu ni mpira.”

“Kila mchezo unahitaji mbinu yake ya ushindi, hivyo wanapopewa majukumu wanatimiza kwa kushirikiana, kabla ya mchezo huwa ninaangalia wapinzani wanafanyaje na nina wachezaji wa aina gani, hapo tunakwenda kuwakabili,” amesema Nabi.

Aziz Ki alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu huu, akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mabingwa wa Soka Ivory Coast ASEC Mimosas.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here