Home KITAIFA NABI:TUMETUMIA MUDA MWINGI KWENYE NDEGE KULIKO UWANJANI

NABI:TUMETUMIA MUDA MWINGI KWENYE NDEGE KULIKO UWANJANI

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa ratiba ni ngumu lakini hawalalamiki huo ni ukweli.

Nabi amebainisha kuwa wametumia muda mwingi kwenye ndege kuliko muda wa kufanya maandalizi kwa mechi iliyo mbele yao.

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Nabi amesema:-“Ratiba yetu ni ngumu sana. Tumemaliza muda mwingi kwenye Ndege kuliko Uwanja wa mazoezi. Tangu Jumatano hatujafanya mazoezi kujiandaa na mchezo huu.

“Tumefika Mwanza usiku na tuna siku moja tu ya mazoezi. Hii sio rafiki kwa afya ya mwili wa wachezaji.

“Hatuko hapa kulalamika lakini tunaamini Viongozi wa mpira wetu jambo hili kwa wakati mwingine wanatakiwa kulitazama kwa jicho tofauti”.

Yanga imetoka Tunisia ilipokuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain na ilipata ushindi wa bao 1-0 na kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here