Home KITAIFA RASMI: SIMBA NA YANGA KUPIGWA TENA MWEZI UJAO

RASMI: SIMBA NA YANGA KUPIGWA TENA MWEZI UJAO

0

LIGI Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara msimu huu wa 2022/23, inatarajiwa kuanza Desemba 5, huku ‘dabi’ ya watani wa jadi, Simba Queens na Yanga Princess wakitarajiwa kupambana Desemba 16, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF), Mabingwa Watetezi, Simba Queens, watakata utepe wa msimu mpya wa ligi hiyo Desemba 5 watakapocheza dhidi ya JKT Queens kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju, Dar es Salaam, huku Yanga Princess ikianza ligi siku inayofuata katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dhidi ya Fountain Gate Princess.

Siku hiyo hiyo kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi, Amani Queens itaikaribisha Baobab Queens, Alliance Girls itakuwa Uwanja wa Nyamagana kucheza dhidi ya Ciassia Queens, wakati The Tigers Queens na Mkwawa Queens zitakipiga kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Raundi ya pili ya ligi hiyo kwa mujibu wa ratiba hiyo, itaanza Desemba 9 wakati The Tigers Queens itaikaribisha Simba Queens kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Alliance Girls itakuwa nyumbani, Nyamagana kuipokea JKT Queens, wenyeji Boabab Queens watakuwa Jamhuri Dodoma kuikaribisha Ciassia Queens, Yanga Princess itakuwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kucheza dhidi ya Mkwawa Queens na Amani Queens itacheza na Fountain Gate Princess kwenye Uwanja wa Ilulu.

Desemba 16, mwaka huu Simba Queens itacheza dhidi ya Yanga Princess, lakini mpaka sasa uwanja bado haujajulikana, na unatarajiwa kutangazwa baadaye.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here