Home KITAIFA RUVU SHOOTING MAMBO MAGUMU

RUVU SHOOTING MAMBO MAGUMU

0

Kocha Mkuu wa Timu ya maafande wa Ruvu Shooting Charles Boniphace Mkwasa Masta,amesema kwa sasa kikosi chake kinapitia wakati mgumu kutokana na matokeo yasiyoridhishwa.

Ruvu Shooting kwa sasa wapo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu ya NBC,wakicheza mechi 10 ambapo wameshinda mechi 3,sare mechi moja huku wakipotezza mechi 6.

Charles Mkwasa amekwenda mbali zaidi na kutoa lawama kwa washambuliaji wake ambao wameshinda kumpa matokeo mazuri ambapo katika mechi 5 za mwisho Ruvu Shooting wameambulia alama 2 tu. Kwa sasa Rashid Juma na AbalKassim Suleimani kila mmoja ana mabao matatu ligi kuu.

Mkwasa ana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa Ruvu Shooting maarufu Barcelona ya Bongo inarudi katika mtiririko wa ushindi maana nafasi waliyopo sioo nzuri kwani timu ambayo inakamata nafasi ya mwisho Ihefu FC ina alama 5 ambazo wanaweza kuifikia Ruvu Shooting.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here