Home KITAIFA SHAFFIH DAUDA: HAKUNA KAMA SURE BOY NA NDEMLA NCHI HII

SHAFFIH DAUDA: HAKUNA KAMA SURE BOY NA NDEMLA NCHI HII

0

Mchambuzi maarufu wa soka nchini, Shaffih Dauda ameonyesha kufurahishwa na viwango vya wachezaji katika nafasi za kiungo ambao ni wazawa.

Hii ni baada ya wachezaji kama Said Ndemla wa Singida Big Stars na Salum Abubakary ‘Sure Boy’ wa Yanga kuonyesha viwango vya hali ya juu katika siku za hivi karibuni.

“Kabla ya Mtanzania mwingine kuonesha mpira mkubwa sana eneo la Kiungo pale Tunis wa kuitwa @sure8boy basi kuna Mtanzania mwingine Kiungo wa mpira aliuwasha sana pale Singida anaitwa @ndemla13.

“Kuna kizazi fulani kilitokea hapa nchini, kilizalisha Viungo wengi sana ambao wengi kwasasa ndio uti wa mgongo wa timu zao, mpira mzuri sana wanaupiga, binafsi nafurahishwa sana na wazawa msimu huu.

“Ilikuwa siku ya kuipa heshima bendera na rangi zake nne, good game kwa Sure Boy na Said Khamis Ndemla, moja kati ya kizazi bora sana cha viungo,” amesema Shaffih.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here