Home KITAIFA SHAFIIH DAUDA KATOA USHAURI HUU KWA FEI TOTO

SHAFIIH DAUDA KATOA USHAURI HUU KWA FEI TOTO

0

Mchambuzi maarufu wa Soka nchini na mtangazaji wa Clouds Media, Shaffih Dauda amelishauri benchi kla ufundi la Klabu ya Yanga kumrejesha kiungo wake mshambuliaji, Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika nafasi yake ili aweze kuwa na mchango mkubwa katika kikosi hicho na kupata matokeo.

Kauli hiyo ya Shaffih inakuja baada ya Yanga wakiwa nyumbani katika Dimba la Mkapa jana kutoa sare ya bila kufungana na Club Africain ya Tunisia kwenye mchezo wa mtoano kuwania kufuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kwa siku za hivi karibuni, hasa baada ya ujio wa Aziz Ki, Kocha Mkuu wa Yanga amekuwa akichezesha Feisal nafasi ya namba 8 badala ya namba 10 aliyokuwa akicheza msimu uliopita na kuisaidia pakubwa timu yake.

“Feisal Salum ana eneo lake ndani ya uwanja ambalo analimudu vyema, anafunga sana akitumika kama 10, ni bora sana akicheza nyuma ya mshambuliaji lakini bahati mbaya sana hapewi sana nafasi ya kucheza eneo lile na anaeyepewa ana mabao mawili tu kwenye ligi na moja ni la set piece.

“Mpeni Feisal eneo lake, atawasaidia sana na ndie mwenye mabao mengi zaidi kikosini kwenye ligi,” amesema Shaffih.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here